Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeLifestyle+FashionLulu naye mgonjwa?
| + -

Lulu naye mgonjwa?

Friday, 23 March 2012 07:43 Deiwaka World News - Lifestyle+Fashion
Print PDF

Lulu naye mgonjwa?

Mwigizaji ‘sura ya mauzo’ Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amezidiwa ghafla ukumbini katika sherehe ya mwaka mmoja ya kuzaliwa kwa Klabu ya Bongo Movie.

Tukio hilo lilijiri usiku wa Machi 16, mwaka huu katika Ukumbi wa Business Park Kijitonyama, Dar ambapo ndipo ilipofanyikia shughuli hiyo.

Tofauti na alivyozoeleka, Lulu alipofika katika sherehe hiyo alionekana kuwa mpole, asiye na mbwembwe, hali iliyowafanya watu wengi kuamini siku hiyo alikuwa na matatizo yanayomsumbua.

“Mh! Jamani Lulu leo katulia kupita maelezo, si bure atakuwa na kitu kinamsibu kwa sababu kwa utulivu alio nao utadhani hayupo vile,” alisema dada mmoja aliyekuwa meza moja na Lulu.

Lulu alipoulizwa kulikoni kuwa kimya kiasi hicho, alisema yupo sawa na hakuwa na matatizo yoyote lakini siku hiyo alikuwa na utulivu wa hali ya juu huku akionekana kuchezea simu yake ya mkononi.

Wakati sherehe hiyo ikielekea ukingoni, mtu wa karibu alimtonya paparazi wetu kuwa, alimuona Lulu akiondolewa ukumbini kwa kubebwa.

Mtu huyo alidai kuwa Lulu alitolewa nje ya ukumbi na jamaa mmoja aliyekuwa akimsaidia huku akionekana kulegea mwili.

Hata hivyo, baadaye usiku huo, alionekana kwenye klabu ya New Maisha, Masaki jijini Dar, lakini pia hakuwa mchangamfu.

Kesho yake (Jumamosi), ripota wetu alimtafuta Lulu kwa njia ya simu ili kumjulia hali yake ndipo alipofunguka:

“Usiku nilipatwa na hali fulani hivi mbaya, mwili uliishiwa nguvu ghafla ndiyo maana huyo mtu alikuambia nilizidiwa.

“Nakumbuka kuna mwanaume alinisaidia kunitoa nje, hata hivyo, nimeamka poa lakini inabidi nikacheki afya kama ulivyosema ni muhimu.”