Abdul Aboubakar Chende kutoka A Town, mwanamuziki wa Hip Hop anayesadikika kuwa na umri mdogo kuliko wote baada ya kutimiza ndoto zake tatu sasa anaenda kwenye ya nne ambapo mwishoni mwa wiki hii mbele ya washkaji zake na mtandao wa Deiwakaworld amethibitisha kutamani kupanda ndege!
Umeona bwana?
Dogo mwanzoni alikuwa hana hata imani kwamba ipo siku atakuja kukutana na Raid lakini kakutana na Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na wakala snepu, alitamani kutoka kimuziki, tayari kitaani anasikika na single zake mbili, ya kwanza akiwa kamshurikisha Tundaman na ya pili akiwa na Godzilla wa salasala.
Umetusoma mpaka hapo ndoto ya tatu sasa Dogo akatamani shule, na sasa hivi ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari Makongo kidato cha kwanza. Sasa hii ya ndege ni ndoto ya nne ambapo dogo kadiriki kusema hata kwa shoo ya bure, ili mradi tu usafuru uwe ndege, ..yeye yuko radhi.
Kazi kwa wadau na mapromota kijana kutoka Ngarenaro, a.k.a Ololooooo, katamani mwewe, kama kuna shoo mbele mbele nini, muwekeni tuone...
Click here for TUMA Registrations.