Hatimaye majina ya wanamuziki wa kundi la Five Stars Modern Taarab waliofariki usiku wa kuamkia leo katika ajali mbaya ya basi yamefahamika. Waliofariki katika ajali ya Bendi ya Five Star ni pamoja na Issa Kijoti, Omar Tolu, Haji Babu, Sheba Juma, Omar Hashim, Tizo Mgunga, Hamisa Mipango, Husna Mapande, Samir Maulid, hasan Ngereza, Rama Kinyoya, na Nasoro Madenge.
Walionusurika ambao wako hospitalini, ni Bi Mwanahawa Ally kutoka kundi la East African Melody ambaye alialikwa katika onesho hilo, Susan Benedict, Zena Mohamed, Samila Rajab, na Mwanahawa Hamis.
Kwa mujibu wa walionusurika, dereva wa basi dogo walilokuwa wamepanda alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kasi sana, na alijikuta akilivaa lori lililokuwa limeegeshwa katika harakati za kukwepa lori jingine ambalo alikuwa agongane nalo uso kwa uso alipokuwa aki"overtake".
Mipango ya kusafirisha miili ya Marehemu pamoja na majeruhi kuelekea jijini Dar inaendelea mchana huu, mungu alaze pema peponi roho za marehemu, Amen.
Click here for TUMA Registrations.