
Sababu ya Sugu Kuikataa Fiesta Mbeya
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu’ ameweka wazi kuwa Tamasha la Fiesta halihitajiki kwa maslahi ya watu wa kawaida na wasanii wenyewe. Kwa takriban wiki moja sasa, Sugu ambaye anabeba ujiko kwa uasisi wake wa Hip Hop na Bongo Fleva ndani ya Bongoland, amekuwa kwenye gumzo na baadhi ya wadau kuhusiana na uamuzi wake huo wa kuipotezea Fiesta.
Baada ya maneno ya hapa na pale, Sugu amefunguka kuwa Fiesta haihitajiki kwa sababu tangu imeanzishwa haijawahi kutoa matunda yoyote kwa wasanii.
Sugu ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo alisema: “Kuna watu hawajui haya mambo. Ninaposema wasanii wananyonywa kupitia Fiesta, namaanisha kuwa kuna mchezo mchafu unaoendelea.
“Mimi naujua huu muziki, ni sisi ambao tumeweka misingi ya kuufanya umkomboe msanii wa Tanzania. Tumeubadilisha ili uwe ajira kwa vijana wenye vipaji lakini kilichopo sasa ni kwamba baadhi ya wawekezaji ndiyo wananufaika wakati wasanii wana hali duni.
“Sizungumzi kama mbunge tu, nalisemea hilo nikiwa Waziri Kivuli wa wazara husika, kwa hiyo ni kitu kilichopo ndani ya himaya yangu. Siwezi kuona hili tatizo linaendelea. Ubabaishaji wa Fiesta inabidi ukome mara moja.
Â
“Nimesema Fiesta haihitajiki Mbeya kwa sababu ni jimbo ambalo ninaliongoza. Sihitaji kuona watu wangu wanadanganywa. Tangu hiyo Fiesta ianze zaidi ya miaka 10 sasa, sijaona faida kwa msanii yeyote wa Mbeya.
“Waliopo Dar es Salaam ndiyo kwanza wanazidi kunyonywa. Ni mambo ambayo tunahitaji kuyamulika kinaga ubaga. Hapa hatujadili chuki binafsi, isipokuwa tunaangalia faida. Fiesta ina faida gani kwa Watanzania? Sioni faida zaidi ya kelele.
“Hivyo msimamo huu una lengo la kumtetea msanii wa Mbeya na Tanzania kwa jumla. Tuache ubabaishaji, hakuna ajira ambayo imewahi kuletwa na Fiesta, zaidi ya watu wale wale kunufaika kwenye migongo ya wasanii.â€
Click here for TUMA Registrations.