Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kuwa kipo tayari kwenda uchanguzi mdogo baada ya kumfukuza uanachama Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda.
Kwa siku kadhaa sasa, Shubuda ameingia kwenye mgogoro na chama hicho baada ya kutoa hoja bungeni inayokinzana na msimamo wa chama chake kuhusu suala la posho za vikao vya bunge.
Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alisema kuwa Chadema ipo tayari kwenda kwenye uchaguzi mdogo kuliko kuendelea kumlea mbunge msaliti kama Shubuda.
“Kama Shubuda anaona Chadema ni mbaya arudi alikotoka au kama anaona atageuka jiwe atafute sehemu nyingine ya kwenda,†alisema Lissu.
Â
Aliendelea kusema kuwa Shubuda amekuwa akizungumza lugha chafu na kauli za matapishi ambayo yanakichafua chama.
Â
“Shubuda hana lolote zaidi ya matapishi. Hana jipya, ni kama wale wa jana na juzi waliokuwa wakisema kuwa Chadema ni chama cha familia ya Mtei (Edwin) na mkwewe Mbowe (Freeman), ni cha wachaga. Hana jipya zaidi ya hayo,†alisema Lissu.
Wakati Chadema kimekataa posho za vikao bungeni, Shibuda aligeuka msimamo huo wa chama chake na kutaka ziendelee ikiwezekana ziongezwe kufikia shilingi 500,000 badala ya sasa ambapo ni shilingi 70,000 kwa siku.