Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeBusiness+PoliticsZitto Awa Mmbogo Kuambiwa Anajengwa Na JK
| + -

Zitto Awa Mmbogo Kuambiwa Anajengwa Na JK

Tuesday, 12 July 2011 10:44 Na Mwandishi Wetu News - Political Issues
Print PDF

Zitto and JKMbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema kuwa hajengwi na mtu kisiasa isipokuwa anajijenga yeye binafsi pamoja na nguvu ya umma.

Zitto, aliye Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, aliyasema hayo akijibu habari kubwa iliyoandikwa na gazeti la Tanzania Daima la leo lenye kichwa kinachosema “Kikwete amjenga Zitto.”

Katika maelezo ya gazeti hilo ambalo linamilikiwa na Mwenyekiti wa Chadema aliye pia Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, ukaribu wa Zitto na JK umekuwa na viulizo vingi.

Gazeti hilo lilieleza kuwa Zitto atapoteza watu kwa ukaribu wake na JK kwa maelezo kwamba kiongozi huyo umaarufu wake umeshuka.
Zitto kupitia ukurasa wake wa Facebook, alisema kuwa kama habari hiyo ingeandikwa na gazeti lingine asingeshangaa lakini anaona ajabu kuandikwa na Tanzania Daima ambalo linamilikiwa na kiongozi mkuu wa chama chake.

“Tanzania Daima Leo habari yao kuu ni 'Kikwete amjenga Zitto'. Nisingeshangaa Kama habari hii ya kizushi ingetoka Jamboleo. Nashangaa habari hii kuandikwa na gazeti linalomilikiwa na Kiongozi Mkuu wa Chama changu. Sijengwi na mtu, NAJENGWA NA UMMA,” alisema Zitto.
Hata hivyo, baadaye baadhi ya marafiki zake walitoa maoni yao na mmoja wao alimwambia alifanya haraka kueleza hisia zake kuhusu Tanzania Daima, kwani inaweza kuongeza migogoro.

Jibu hilo lilimfanya Zitto awe mbogo na kusisitiza kwamba ana haki ya kufanya hivyo kwa sababu amevumilia muda mrefu.

joomla stats

Deiwaka Tweets