Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeMusicSugu Aitoa Nishai Fiesta Mbeya Bila Stress
| + -

Sugu Aitoa Nishai Fiesta Mbeya Bila Stress

Wednesday, 13 July 2011 17:52 Na Ripota Wetu News - Music
Print PDF

Suma G (kulia) na Soggy wakikamua jukwaani huku nyomi la Burudani Nyumbani likijieleza.Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi "Sugu" wikiendi iliyopita alitumia uzoefu wake katika anga ya burudani Bongo na kulitoa kapa Tamasha la Fiesta ambalo huendeshwa kila mwaka.

Jumamosi iliyopita, Fiesta walijaribu kuliungurumisha kwenye Uwanja wa Sokoine lakini walikula za uso, tofauti na matarajio yao.

Sugu ambaye ni muasisi wa Bongo Fleva, alipinga Fiesta kufanyika Mbeya kwa sababu halina faida kwa wakazi wa Mbeya na wasanii kwa jumla.

Alisema, Fiesta ipo kwa miaka 10 sasa lakini imeshindwa kubadili maisha ya wasanii na haijachochea ajira kwa namna inavyotakiwa zaidi ya waandaaji kuvuna fedha.

Hata hivyo, waratibu wa Fiesta walishikilia msimamo wao na kusisitiza kufanya tamasha hilo.

Kutokana na msimamo huo wa Fiesta na msukumo wa Sugu, liliandaliwa tamasha la wazi la bure ambalo lilitwa Burudani Nyumbani – No Stress.
Kwa mujibu wa tathmini ya matamasha hayo, Burudani Nyumbani lilitisha kwa sababu lilifunga nyomi si la kitoto wakati lile la Fiesta lilibaki na aibu.

Kwa tathmini hiyo, Sugu aliweza kulichapa bakora Fiesta, huku wakazi wengi wa Mbeya wakitoa ahadi kwamba mwakani ni bora lisirudi tena, kwani aibu itakuwa zaidi ya hapo

Mkoloni akitoa holler, nyuma yake ni nyomi lilitinga kwenye Burudani Nyumbani No Stress.

 

Sogi akiwa amepozi, nyuma yake ni nyomi la Buradani Nyumbani No Stress.

 

Sugu siku alipokula kiapo bungeni, Novemba mwaka jana.