Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeBusiness+PoliticsZitto Akomalia Ufisadi wa Shilingi Bilioni 200
| + -

Zitto Akomalia Ufisadi wa Shilingi Bilioni 200

Friday, 15 July 2011 01:28 Na Ripota Wetu News - Political Issues
Print PDF

Zitto And MboweMbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe ametaka ufanyike uchunguzi na ikiwezekana ielezwe sababu ya malipo ya kifisadi ya zaidi ya shilingi bilioni 200 kutoka Benki Kuu kwenda Nedbank ya Afrika Kusini.

Zitto ambaye ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani alisema bungeni jana kuwa Kampuni ya Meremeta ilikopa shilingi bilioni 16 (dola milioni 10) kutoka

Nedbank lakini serikali ilipoamua kulibeba deni hilo, ililipa zaidi ya shilingi bilioni 200 sawa na dola milioni 132.

Kwa mujibu wa Zitto, serikali ililipa deni hilo ikiwa ni mara 13.2.

“Ni kwa nini malipo haya yamefanyika? Kama ni kwa maslahi ya umma tuelezwe,” alisema Zitto.

 

Aliendelea kusema kuwa anazo nyaraka zinazoonesha kuwa Meremeta ilikopa shilingi bilioni 16 wakati serikali imelipa zaidi ya shilingi bilioni 200.
“Nimewaandikia barua Nedbank waeleze ni kwa nini wamepokea malipo hayo lakini hawajanijibu. Mimi sijachoka, nahitaji kujua kiini cha malipo haya,” alisema Zitto kwa kujiamini.

 

Alisema, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh alikwenda Hazina kwa lengo la kuchunguza kiini cha malipo hayo lakini alinyimwa ushirikiano.

AOMBA KAMATI TEULE

Bungeni jana jioni, wakati bunge lilipoketi kama kamati kupitisha bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Zitto alisimama na kuliomba bunge lifanye uchunguzi kuhusu malipo hayo.

Hata hivyo, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugayi alimtaka Zitto awasilishe hoja yake kwa maandishi kabla ya kufanyiwa kazi na ofisi ya spika.