Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu’ amesema kuwa mipaka ya nchi siyo salama ndiyo maana wasomali wametapakaa kila kona ya nchi.
Sugu, aliyasema hayo wakati bunge lilipoketi kamati ya bunge zima kujadili na kupitisha bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Alisema, mipaka ya nchi siyo Salama ndiyo maana Wasomali wametanda kuanzia kaskazini mwa nchi mpaka Kyela, Mbeya ambako ni kusini.
“Wasomali ni watu hatari, kule Somalia kuna tishio la vikundi vya kigaidi kama Al-Shabab. Sasa kama watu hao wanaweza kupenya na kuingia Tanzania kwa wingi ni vipi tutasema tupo salama?†alihoji Sugu.