Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeBusiness+PoliticsWabunge wafundishwa kujilinda na Ukimwi
| + -

Wabunge wafundishwa kujilinda na Ukimwi

Monday, 08 August 2011 03:23 Deiwaka World News - Political Issues
Print PDF

Wabunge wafundishwa kujilinda na Ukimwi

Na Ripota Wetu

Wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamepewa somo la kujikinga na Ukimwi.

Tume ya Kupambana na Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ndiyo iliyotoa semina hiyo ambayo ilifanyika bungeni jana kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa.


Chanzo chetu kilisema kuwa wabunge wote waliohudhuria walipata bahati ya kupata mafunzo kuhusu namna sahihi ya kujilinda na Ukimwi kwa manufaa yao na wananchi wanaowawakilisha.

“Tumepata semina, ilikuwa nzuri na kuna mambo mengi ambayo tumejifunza,” kilisema chanzo chetu ambacho ni mbunge kisha kikaongeza:

“Ni vizuri kupata mafunzo kama hayo, nasi tutaenda kuyatumia ipasavyo ili tusipate maambukizi ya Ukimwi, vile vile tutawapa muongozo mzuri wapiga kura wetu.”

Hata hivyo, mbunge mwingine (jina tunalo) aliponda semina hiyo kwa kile alichodai kwamba ni matumizi mabaya ya fedha.

“Wabunge ni viongozi, ni ajabu mtu anakuwa kiongozi wa watu halafu awe hajui jinsi ya kujilinda na Ukimwi. Hiyo siyo sawa, haya ndiyo matumizi mabaya ya fedha ambayo tunayazungumzia kila siku,” alisema mbunge huyo.

Aliongeza: “Nadhani TACAIDS wanatakiwa kuelekeza nguvu zao vijijini, huko kuna watu ambao kweli wanahitaji elimu, siyo hapa mjini. Mbaya zaidi kwa wabunge.”