Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeSportYanga full kujiamini Sudan
| + -

Yanga full kujiamini Sudan

Monday, 08 August 2011 03:29 Deiwaka World News - Sports News
Print PDF

Yanga full kujiamini Sudan

Na Ripota Wetu

Klabu ya Yanga ipo salama salmini nchini Sudan na leo jioni inatarajiwa kujitupa uwanjani kucheza moja ya mechi zake za kirafiki.

Yanga, iliondoka jana kwa ndege kuelekea Sudan ambako wana vibarua viwili vya mechi za kirafiki jiji Khartoum.


Leo usiku, Yanga itakipiga na El Hilal kabla ya kumalizana na El-Mereikh katika mchezo wa mwisho nchini humo.

Chanzo chetu ndani ya Yanga kimepasha kuwa timu ipo vizuri na kwamba wachezaji wamejipanga kuonesha uwezo ili kumshawishi Kocha Sam Timbe kuwapanga kwenye mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Simba Agosti 17, mwaka huu.

“Hakuna mtu ambaye hapendi kupangwa kwenye mchezo huo. Kucheza dhidi ya Simba inahitaji kuwa na sifa ya ziada, kwa hiyo kila mmoja anataka kuonesha uwezo wa ziada ili kumshawishi kocha,” kilisema chanzo chetu.

Msemaji wa Yanga, Lous Sendeu alimueleza ripota wetu jana kuwa safari ya Sudan ina malengo makubwa mawili lakini kubwa ni kupata mazoezi ya juu kabla ya kuikabili Simba.

“El-Mereikh na El-Hilal ni timu kubwa, kwa hiyo kujipima nazo ni kupata mazoezi mazuri kabla ya kuikabili Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Hisani. Lengo la pili ni kukiandaa vizuri kikosi chetu kabla ya kuanza Ligi Kuu msimu mjao,” alisema Sendeu.

Â