Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeBusiness+PoliticsSugu: Akina Ruge wanakuharibia JK kwa vijana
| + -

Sugu: Akina Ruge wanakuharibia JK kwa vijana

Sunday, 14 August 2011 05:32 Deiwaka World News - Political Issues
Print PDF

Sugu: Akina Ruge wanakuharibia JK kwa vijana

Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amethibitisha kiwango chake bungeni kwamba siyo mchezo. Hajaenda kuuza sura wala kucheka baada ya jana kuwasha moto mkali ikiwemo kuwataja waziwazi watu wanaotuhumiwa kwa kufanya ufisadi kwenye muziki wa kizazi kipya.



Sugu akizungumza kwa hisia kali bungeni, alisema kuwa kama vijana wa Tanzania watawezeshwa, wana nafasi kubwa ya kuondokana na dhana ya kufikiria hawawezi kuondokana na umaskini bila kuuza unga.

Aliponda staili ya kuchangamkia kwenye tasnia ya sanaa Bongo kwamba haufai kwa sababu unaruhusu fedha nyingi kwenda na maji.

Alisema, utafiti uliotolewa mwaka jana na wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam umeonesha kuwa serikali inapoteza mapato kwenye muziki wa kizazi kila mwaka zaidi ya shilingi bilioni 90. Na hii ni kwa sababu haiweki mkazo kwenye usimamizi wa utamaduni.

“Chombo cha kusimamia sanaa nchini, Basata, hakina fedha za utekelezaji wa maendeleo ya sanaa. Wanapewa tu hela za mishahara. Sanaa haiwezi kuendelea,” Sugu.

“Mheshimiwa Spika, haiwezekani vijana wa taifa hili wafikirie kwamba hawawezi kutajirika bila ya kuuza unga. Hawapendi ila mazingira yanayotengenezwa na wajanja na wajanja wachache yametufikisha hapa.

Hawa wanaitumia Ikulu kuikandamiza fani (Bongo Fleva) na wasanii wake, wameiteka nia njema ya Rais Jakaya Kikwete ya kuwakomboa wasanii,” alisema Sugu na kueleza kuwa adui mkubwa wa Bongo Fleva ni Mkurugenzi wa Masoko wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

Sugu alisema Ruge ndiye anayemharibia JK kwa vijana kwa sababu mtaani anaonekana siyo rafiki wa vijana wakati amejitahidi kufanya kitu lakini amekivuruga.

“Suala la studio ya rais ndiyo Dowans kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya. Mnapotosha nia njema ya rais kusaidia huu muziki, mnamchoresha tu mtaani.

“Siku moja nilikuwa nazungumza na Miraji Kikwete (mtoto wa JK), naye analalamika, mimi nikamuuliza lakini huyu rais si dingi wako? Nikamwambia zungumza, mwambie akina Ruge wanamyeyusha,” alisema Sugu.

Alisema, kuwa studio ya kuboresha muziki kwa wasanii wa Bongo Fleva imehodhiwa na taasisi binafsi ya THT (Tanzania House of Talent) na nyumba iliyotolewa na rais kwa ajili ya kuiweka studio hiyo nayo imehodhiwa na THT, hivyo alisisitiza kuwa huko ni kumpaka matope rais.

Aliongeza, si vema rais afanya kazi na mtu mmoja mmoja au atumie fedha za wananchi kwa maslahi ya taasisi binafsi, kwa hiyo alishauri studio ya wasanii ipelekwe Basata ambako wahusika watajua waiweke wapi kwa ajili ya maendeleo ya wanamuziki wote.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emanuel Nchimbi alisema studio iliyotolewa na rais siyo ya THT ni mali ya Fleva Unit lakini Sugu alihoji Fleva Unit ni nini kwa sababu imewahi kupelekwa Basata isajiliwe kama chama cha wanamuziki wa kizazi kipya ikanyimwa.

“Mheshimiwa spika, hii Fleva Unit ni kampuni, imesajiliwa kwa msajili wa makampuni kwa sababu Basata waliinyima usajili kwa maana tayari kuna chama cha wasanii wa muziki wa kizazi kipya kinaitwa Tanzania Urban Music Association (Tuma) lakini hakijapewa hiyo studio kwa sababu hakina watu wa kumkutanisha na rais,” Sugu.

Sugu alisema, mwanzoni mwa miaka ya 2000, msanii mmoja tu alikuwa akifika mkoani kufanya shoo hali ilikuwa ikibadilika, msafara wa balloon (magari) kama sita, ya msanii na wapambe wake, hivi sasa wanakuja Dodoma wasanii 20 lakini hata pikipiki moja huioni.

Mfumo unawapa wadosi (wasambazi) fursa ya kuwanyanyasa wasanii alisema: “Miaka ya nyuma wadosi walikuwa anatufuata baa za Sinza tunajadili biashara, wanatunyenyekea lakini sasa hivi wasanii wakubwa wanapangwa foleni saa 10 kwa wahindi wanangoja kuzungumza mkataba.

“Mdosi akitokea hiyo inakuwa faraja kwa msanii, ameshaharibika kisaikolojia, kwa hiyo hata mazungumzo ya kimkataba yanakosa viwango kwa sababu msanii ameshaathirika kisaikolojia.

“Mimi nimetoka huko, hakuna hela tena. Wasanii wana hali mbaya, hivi serikali inataka kila kijana ili awe tajiri auze madawa ya kulevya? Mfumo uliopo ni unyonyaji, hii fursa ya muziki wa kizazi kipya ambayo imejitokeza nayo inachezewa, wasanii wanaibiwa. Shoo hakuna, mwaka mzima msanii anasubiria shoo mbili za Fiesta na College Bush.”

Kwa upande mwingine, Sugu aliwaponda ma-marketing manager wa makampuni mbalimbali kuwa wamekuwa wakisababisha wasanii waendelee kunyonywa.

Alikoroma: “Nawaambia hawa ma-marketing manager wa makumpuni mbalimbali yanayodhamini matamasha ya burudani nchini. Hivi huu ni uzalendo gani? Anamsainia malipo ya dola 400,000 (shilingi milioni 640) msanii kutoka nje, wakati msanii wa nyumbani analipwa shilingi 200,000 na bado kwenye shoo huyo msanii wa nje anafunikwa na wa nyumbani.”

Kuhusu kodi, Sugu aliwaka: “Kipindi fulani nilikwenda Marekani, kule wakaniambia haiwezekani mkongwe umekuja ni lazima ututumbuize. Nikafanya shoo ya kufa mtu, nikalipwa dola 2,000 (shilingi milioni 3.2). Asubuhi nikapigiwa simu natakiwa nilipe kodi. Yaani nchi kubwa kama Marekani inanidai kodi kwa dola 2000 nilizolipwa.

“Hapa Tanzania msanii anatoka nje ya nchi analipwa dola 400,000 (shilingi milioni 640) anaondoka nazo zote na kodi halipi. Tanzania ina uchumi mkubwa kiasi gani?”