Gervinho alipozipiga na Barton
Â
Joey Barton alimkoromea Gervinho kwenye Uwanja wa St James' Park jana, mwisho walizipiga.
Barton ambaye ni mchezaji mkorofi kikosi cha Newcastle, alimtuhumu Gervinho kwamba alijiangusha ili Arsenal ipewe penalti.

Gervinho, alianguka ndani ya boksi la 18, kufuatia kuchezewa ‘takolin’ na beki wa Newcastle, Cheik Tiote.
Baada ya Gervinho kuanguka, Barton alimvaa na kumvuta, akamsukuma kisha akamwita muongo lakini mwisho mshambuliaji huyo raia wa Ivory Coast alijibu mapigo kwa kumpiga kofi kichwani.
Alipopigwa kofi, kiungo huyo wa The Toon ‘Newcastle’ alisalimika na kumuacha Gervinho akitolewa nje kwa kadi nyekundu, hivyo kuiacha Arsenal pungufu.
Mchezo huo, ulimalizika kwa suluhu (0-0), hivyo kuzifanya timu hizo kufungua Ligi Kuu ya England kwa pointi moja kila moja.

