Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeBusiness+PoliticsMwandosya kuipa ‘bai bai’ serikali ya JK
| + -

Mwandosya kuipa ‘bai bai’ serikali ya JK

Monday, 22 August 2011 17:29 Deiwaka World News - Political Issues
Print PDF

Mwandosya kuipa ‘bai bai’ serikali ya JK

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mark Mwandosya anahitaji kupumzika kwa muda mrefu, kwa hiyo majukumu ya kiserikali ni mazito kwake.


Kutokana na hali hiyo, daktari wake nchini India amemshauri aandike barua ya kuachia ngazi na vyanzo vinasema kuwa ameshaanza kuufanyia kazi ushauri huo.

Pamoja na taarifa iliyotolewa leo bungeni kusisitiza kuwa Mwandosya anaendelea vizuri, vyanzo vinasisitiza kuwa kiongozi huyo ametakiwa kupumzika.

“Barua ipo tayari na wakati wowote mambo yatakuwa wazi. Siyo siri kwa sasa ni ngumu kuwajibika inavyotakiwa,” alisema mtoa habari wetu na kuongeza:

“Unajua afya ni muhimu, hata hao wananchi anataka kuwatumikia hawezi kuwafanyia kazi zao ipasavyo ikiwa atakuwa anaumwa.”

Gazeti moja la leo, liliropita kuwa Mwandosha ameshaandika habari ya kujiuzulu.

Mwandosya, yupo India akiendelea na matibabu ya mgogo.