Nargis afanyiwa Kitchen Party, ndoa yanukia
Miss Ilala 2003, Nargis Mohamed amefanyiwa sherehe ya kumfunda (kitchen party) na Mungu akipenda, kuanzia Jumamosi ijayo ataanza kutambulika kama mke wa mtu.

Nargis, alifanyiwa kitchen party kwenye Ukumbi wa Karemjee, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na warembo mastaa wakubwa nchini.
Mbali na kuhudhuriwa na mastaa hao, sherehe hiyo ilipambwa na mambo mbalimbali ya kifahari kuonesha kuwa kila kitu kiliandaliwa kikamilifu.
Moja ya vitu ambavyo vilipamba sherehe hiyo ni warembo watatu waliovaa sare za njano, kutinga kwenye sherehe hiyo wakiwa wamesimama kwenye pikipiki, hivyo kuibua cherekochereko za aina yake.
Baadhi ya mastaa waliokuwepo ni Mboni Masimba, Christine John ‘Sinta’, Sauda Mwilima, Salma Msangi na wengineo.
Nargis anatarajiwa kufunga ndoa Jumamosi ijayo na anayetajwa kuwa mchumba wake wa muda mrefu, akifahamika kwa jina la Idd.


