Daktari wa Yanga hajui Cannavaro anaumwa nini
Beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aliumia kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba lakini daktari wa timu hiyo, Juma Sufian amesema kuwa hajui chochote.

Cannavaro yupo nje ywa uwanja kwa wiki kadhaa sasa lakini Sufian amesema, yeye ndiye anapaswa kuwa wa kwanza kujua afya ya mchezaji huyo lakini anasikia taarifa kwenye vyombo vya habari.
“Nasikia Nadir ni mgonjwa, hayo maneno ni kwenye vyombo vya habari, mimi sijui kitu kabisa, nashangaa sana,†alisema Sufian na kuongeza:
“Ni jambo la kushangaza, mimi ndiye daktari wa timu, kwa hiyo kila kitu kinatakiwa kipitie kwangu. Sijui kuhusu Nadir, sifahamu ugonjwa wake, acha niendelee kuona kwenye vyombo vya habari kwa maana kwangu hajaja.â€