Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeSportTFF yajitoa Ligi Kuu
| + -

TFF yajitoa Ligi Kuu

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limedhamiria kujiondoa kuendesha Ligi Kuu Tanzania Bara na badala yake inaandaa menejimenti mpya itakayoisimamia.


Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ‘Ngeta’ amesema kuwa shirikisho hilo linaunda kamati maalum ambayo itasimamia uendeshaji wa ligi hiyo.

Alisema, TFF itabaki na majukumu ya kukuza vipaji pamoja usimamizi wa Timu za Taifa.

“Kamati ndiyo itasimamia kutafuta wadhamini wa ligi pamoja na mambo yote ya uendeshaji wa ligi, uamuzi huu tumeuifikia ili kuendana na wakati uliopo,” alisema Ngeta mbele ya waandishi wa habari leo.

Aliongeza: “Mfumo wa sasa tumeona hatutakiwi kuendana nao. Tunaomba Watanzania wapokee mabadiliko hayo kwa ajili ya mendeleo ya mpira wa miguu Tanzania.”