Diamond amvisha pete ya uchumba Wema
Stadi wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ amethibitisha kwamba hana utani kwa penzi la Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu.

Diamond, amemvalisha pete ya uchumba Wema, hivyo kukamilisha ‘sapraizi’ aliyoahidi kumfanyia mwenzi wake huyo.
Ndani ya Club Maisha, Dar es Salaam jana, Diamond alisimamisha shoo na kumwita Wema jukwaani kisha kutangaza kumfanyia sapraizi mrembo huyo.
Watu wakiwa bize na muziki, waliburudika zaidi na tukio la Diamond kumvalisha pete Wema, hivyo kuwa wachumba rasmi.
Diamond alisema: “Nampenda sana Wema, kwa hiyo mbele ya mama yangu, marafiki zangu na mashabiki wangu waliopo hapa, namvalisha pete hii ya uchumba kuthibitisha kuwa nampenda sana na nitamuoa.â€

Tukio hilo, liliamsha shamra shamra ukumbini na Wema alichukua fursa hiyo kubusu pete aliyovishwa na Diamond kisha akawaonesha mashabiki waliokuwepo kwenye klabu hiyo.
Mbali na tukio hilo, Diamond alifanya shoo ya nguvu kwenye onesho hilo lililopewa jina la Happy Birthday Diamond, kwani jana ndiyo mwanamuziki huyo alitimiza umri wa miaka 22.
