Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeBusiness+PoliticsWikileaks: Steve Jobs amekufa kwa Ukimwi
| + -

Wikileaks: Steve Jobs amekufa kwa Ukimwi

Dunia ikiwa kwenye majonzi ya kifo cha mgunduzi maarufu kompyuta na simu za Apple, Steve Jobs, mtandao wa Wikileaks umechapisha habari za kushtua.


Wikileaks umeandika kuwa Jobs amekufa kwa Ukimwi na kubainisha kwamba wao wana vyeti vinavyothibitisha hilo.

Mtandao huo umeandika kuwa Ukimwi ndiyo sababu ya Jobs kushambuliwa na kansa kabla ya kusababisha kifo chake.

Umeandika kuwa Jobs alipimwa mwaka 2004 na kukutwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Umeeleza kuwa kampuni ya SxCheck ndiyo iliyompima mwanasayansi huyo na kubaini hilo.

Hata hivyo, taarifa hizo za Wikileaks ambazo zimepewa jina la Rekodi za Kitabibu za Steve Jobs, zimepingwa kwa maelezo kuwa zinapikwa ili kumchafua mwanasayansi huyo.

Wanaopinga taarifa hizo za Wikileaks wanabainisha kuwa Jobs hakuwa mtu wa anasa wala mpenda ngono, kwa hiyo tuhuma za Ukimwi ni uongo.

Jobs aliyefariki dunia jana, ndiye mgunduzi wa vifaa mbalimbali vya kompyuta vyenye nembo ya Apple.

Kati ya vifaa hivyo ni pamoja na iPhone, iPad, iPod, iMac na aina mbalimbali za Macintosh.

Jobs, alifariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 56 na pengo lake limetajwa kuwa litaathiri kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kiuzalisha ya Apple.

Vyanzo vinasema kuwa Jobs ndiye alikuwa roho ya Apple, hivyo kifo chake kinamaanisha kuyumba kibiashara kwa bidhaa zenye nembo hiyo, kwani ndizo zilikuwa zinatawala soko kwa sasa.