Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeMusicSugu kuipeleka Anti-Virus Ikulu
| + -

Sugu kuipeleka Anti-Virus Ikulu

Mbunge aliye mstari wa mbele kuupigania muziki wa kizazi kipya, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema kuwa ataipeleka Mix-Tape ya Anti-Virus Ikulu ili Rais Jakaya Kikwete asikilize kilio cha wanamuziki.


Sugu alisema, anaamini JK anajua matatizo ya wasanii kwa juu juu, hivyo atakaposikiliza Anti-Virus Volume 2, ataweza kubaini mambo mengi.

“Ni moja kati ya mambo ambayo nataka niyafanye kuhakikisha wasanii wa muziki wa kizazi kipya wanatambulika vema. Wanacholilia nitakiweka wazi na lazima JK asikilize kilio chao,” alisema Sugu na kuongeza:

“Ndani ya Anti-Virus Volume 2 ndimo kwenye hoja za msingi kabisa kuhusu namna watu wanavyowanyanyasa na kuwaibia wasanii. Hata studio aliyotoa JK kwa ajili ya kuboresha muziki (mastering studio) imetekwa na wajanja. Yote hayo akishasikiliza Anti-Virus atayajua.”