Rose Ndauka awapotezea Wema, Jack Pentzel
Sistaduu anayeuza kunako ulingo wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka amewapotezea waliokuwa mashosti wake, Wema Sepetu na Jacqueline Pentzel.

Rose, Jack na Wema walikuwa wanaunda umoja walioupa jina la Jarowe kwa lengo la kusimama kama kampuni na kutengeneza filamu zao wenyewe.
Hata hivyo, baada ya kutibuana, Rose amesema kuwa hana mpango wa kushirikiana tena na mashosti wake hao.
“Sijui lakini uwezekano wa mimi kushirikiana na wale sioni,†alisema Rose na kuongeza: “Muda huu kila mtu asimame kivyake. Nina kazi nyingi za kufanya kuliko kukaa kutatua migogoro.â€
Alipoulizwa kama atakuwa tayari kumaliza tofauti na wenzake endapo atatokea mtu wa kuwasuluhisha, alijibu: “Sijui, hebu tuone hapo huyo mtu atakapotokea.â€