Alex Ferguson: Sijawahi kupigwa hivi
Kocha wa Manchester United ‘Man Six’, Sir Alex Ferguson, anaugulia maumivu ya kipigo kikali ambacho timu yake ilikipata jana dhidi ya Manchester City cha mabao 6-1.

Ferguson amesema kuwa hajawahi kupata kipigo kikali kama hicho.
Kipigo hicho, ni kibaya kwa Man Six katika kipindi cha miaka 81.
Katika maelezo yake, Ferguson amesema kuwa straika wa Man City, Mario Balotelli ni muuaji. Balotelli (Super Mario), alitusua mawili ya mwanzo, yaliyoichanganya United.
Ferguson alisema: “Ilikuwa ni siku yetu mbaya kuwahi kutokea. Ni matokeo mabaya katika historia yangu. Hata nilipokuwa mchezaji, sifikiri kama niliwahi kufungwa 6-1. Siamini matokeo.
“Nimevunjwa vunjwa, siwezi kuamini. Inatisha. Kuna mambo mengi ya kukatisha tamaa yaliyofuata kwenye chumba cha kubadilishia nguo.â€
Ferguson alisema, timu yake ilikosa utambuzi wa kawaida baada ya kuruhusu mabao matatu kutoka dakika ya 90.
Alisema: "Tulizingatia kushambulia. Matokeo yake ikawa wanatushambulia watatu dhidi ya wawili.
"Wakati huo, nyuma tulibakiza wachezaji wawili wao wakawa watatu na hiyo ilikuwa ni kujitoa mhanga, ni wehu.
"Nilifikiri kutokana na uzoefu wetu, Rio Ferdinand, Patrice Evra wangeweza kuwakabili washambuliaji watatu lakini tulizingatia kushambulia. Wakati mwingine ilitakiwa utambuzi wa kawaida ufanye kazi kwa wachezaji wetu.
"Baada ya kufungwa 4-1 kila mmoja alizingatia kushambulia. Tulipatikana, ilikuwa siku yetu mbaya.â€
Kwa upande wa Kocha wa Man City, Robert Mancini, alisema kuwa kila mchezaji alijitahidi lakini mwisho alimwagia pongezi Super Mario.
“Mario ni mchezaji mkubwa, ana upungufu wa kawaida kutokana na umri wake lakini ukiniambia nichague wachezaji watano bora duniani, Mario ni mmoja wao. Yule ndiye alikuwa chachu ya kusambaratisha United,†alisema Mancini.