Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeSportSimba, Yanga ni vita
| + -

Simba, Yanga ni vita

Oktoba 29, 2011 (Jumamosi inayokuja), nyasi za Uwanja wa Taifa zitakuwa kwenye seleka zito kutokana na mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga.


Ni mechi ya kwanza kwa timu hizo kukutana kwenye mzunguko wa Ligi Kuu mwaka huu.

Mara ya mwisho timu hizo kukutana, ilikuwa wakati wa kuwania Ngao ya Jamii na Simba iliichabanga Yanga mabao 2-0.

Kutokana na vita kali iliyopo, Simba na Yanga kila moja imehama kambi ili kujiwinda na mechi hiyo ambayo inangojewa kwa hamu na wapenzi wa soka Bongo.

Simba ambayo ilikuwa imeweka kambi eneo la Bamba Beach, Kigamboni, Dar es Salaam, imehamia Zanzibar kwa kile ilichodai kuwa ni kukwepa hujuma za watani wao wa jadi.

Ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema: “Tuna dhamira ya kuifunga Yanga, tumehamia Zanzibar ili timu ipate maandalizi mazuri chini ya Kocha Moses Basena.”

Kwa upande wa Yanga, imeelezwa kuwa timu hiyo imekwenda Msumbiji na itakaporudi, itakuwa tayari kuikabili Simba.

Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu amesema: “Hatuna shaka na Simba, kuifunga ni lazima. Tunakwenda Msumbiji kujiandaa, tukirudi tutakuwa kamili kumfunga Mnyama.”