Mtangazaji mwenye jina kubwa Bongo, Maimartha Jesse, amenasa ujauzito.

Habari zinasema kuwa ujauzito huo, umemuongezea furaha Mai ambaye sasa anaweza kutulia kwenye ndoa yake mpya.
Mai, ameolewa na jamaa anayefahamika kwa jina Shah, baada ya aliyekuwa mchumba wake, aliyedumu naye kwa miaka sita, Perfect Kagisa, kufariki dunia.
Hata hivyo, Perfect Diddy alifariki dunia siku chache baada ya kutengana na Mai.
Niuzâ zinapasha kuwa hivi sasa Mai amenenepa na ujazo wa tumbo lake ni mkubwa.
Mai alipopigiwa simu na mwandishi wetu, alijibu: Mwanamke kupata mimba ni jambo la heri, ukizingatiwa mimi nipo kwenye uhusiano unaoeleweka