Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeSportChelsea mbendembende kwa Arsenal
| + -

Chelsea mbendembende kwa Arsenal

Ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani leo, Chelsea iligeuka mbendembende mbele ya Arsenal inayojitahidi kunoa makali baada ya kuanza vibaya Ligi Kuu ya England.


Arsenal, ikicheza kwa kujiamini, imeifunga leo Chelsea katika mchezo ambao ulichukua nafasi kwenye Uwanja wa Stanford Bridge, London.

Chelsea ilipata bao la kwanza kupitia kwa Frank Lampard lakini baadaye nahodha wa Arsenal, alirekebisha na kufanya ubao wa matokeo kusomeka 1-1.

Nahodha wa Chelsea, John Terry, alikandamiza ndoo maridadi na kuifanya timu yake imalize ngwe ya kwanza ikiwa inaongoza kwa mabao 2-1.

Kipindi cha pili, beki wa kushoto wa Arsenal, Clarindo Andre Santos alisawazisha dakika ya 49 kabla ya Theo Walcott kuongeza chuma cha tatu dakika ya 55.

Juan Mata alisawazisha kwa upande wa Chelsea dakika 80 lakini Persie alithibitisha kwamba yeye ni muhimu kwa Arsenal kwa kupachika bao la nne dakika ya 85.

Persie alipiga hat-trick kwa kuiwezesha Arsenal kukamilisha ushindi wa mabao 5-3 dakika ya 92 (dakika ya pili, muda wa nyongeza).