Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeBusiness+PoliticsOparesheni ya Zitto yafanikiwa India
| + -

Oparesheni ya Zitto yafanikiwa India

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, amefanyiwa oparesheni ya kichwa jana ambayo imefanikiwa kwa asilimia 100.


Zitto, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Tanzania Bara, amelazwa kwenye Hospitali ya Apollo iliyopo kwenye Jiji la Bangalore, India ambako alipelekwa na ofisi ya bunge kwa ajili ya upasuaji wa kichwa.

Mbunge huyo ambaye ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, aligundulika kuwa na ugonjwa wa Sinusitis ambao ni uvimbe kwenye vijinafasi wazi kwenye fuvu.

Kwa kawaida, vijinasafi wazi (sinus) ndivyo humuwezesha binadamu kukibeba kichwa chake.

Kwa mujibu wa taarifa ya Zitto, aliyoiweka jana usiku kwenye ukurasa wake wa Facebook, oparesheni ilifanikiwa kwa asilimia 100 na baada ya siku nne, hali yake itatengemaa.

Zitto ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Hesabu za Mashirika ya Umma, amewashukuru ndugu zake, marafiki na Watanzania kwa jumla kwa sala na salamu za kumtakia nafuu.

Kuonesha kuwa Zitto ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Fedha anaendelea vizuri, aliandika leo kwenye ukurasa wake wa Facebook:

“ Leo nimetembelewa na wagonjwa wenzangu waliopo hapa Apollo Bangalore, Mama Kilewo kutoka Bomang'ombe, Hai na Mama Mmari kutoka KCMC, Moshi. Mama Mmari anaondoka leo kurudi nyumbani. Nimefurahi sana.”