Niyonzima atia kiwewe Yanga
Klabu ya Yanga, imeingia na kiwewe, kwa hiyo hivi sasa inahaha kuhakikisha kiungo wake, Haruna Niyonzima anabaki kwa gharama yoyote ile.

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE /* Style Definitions */ table.MsoNormalTable {mso-style-name:"Table Normal"; mso-tstyle-rowband-size:0; mso-tstyle-colband-size:0; mso-style-noshow:yes; mso-style-priority:99; mso-style-qformat:yes; mso-style-parent:""; mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt; mso-para-margin-top:0in; mso-para-margin-right:0in; mso-para-margin-bottom:10.0pt; mso-para-margin-left:0in; line-height:115%; mso-pagination:widow-orphan; font-size:11.0pt; font-family:"Calibri","sans-serif"; mso-ascii-font-family:Calibri; mso-ascii-theme-font:minor-latin; mso-fareast-font-family:"Times New Roman"; mso-fareast-theme-font:minor-fareast; mso-hansi-font-family:Calibri; mso-hansi-theme-font:minor-latin; mso-bidi-font-family:"Times New Roman"; mso-bidi-theme-font:minor-bidi;}
Niyonzima atia kiwewe Yanga
Klabu ya Yanga, imeingia na kiwewe, kwa hiyo hivi sasa inahaha kuhakikisha kiungo wake, Haruna Niyonzima anabaki kwa gharama yoyote ile.
Timu ya APR ya Rwanda ndiyo inayoipa kiwewe Yanga, kwani imeshatangaza kumuwania kiungo huyo kwa gharama yoyote ile.
Katibu Mkuu wa APR, Adrof Kalisa amesema kuwa Niyonzima anahitajika APR na kwamba mamilioni siyo tatizo kutoa ili kumtwaa kiungo huyo.
“Tunamchukua, huku ndiko kwenye maisha mazuri zaidi kwa Niyonzima. Hawezi kukataa kuja huku kwa sababu tutamlipa vizuri na zaidi ya yote Rwanda ndiyo nyumbani kwao,” alisema Kalisa.
Aliendelea kusema kuwa hivi sasa APR imejikita zaidi katika kusajili wachezaji kutoka mataifa mengine mbalimbali na baada ya hapo watarudi kumaliza kazi ya kumnasa Niyonzima.
“Ni mchezaji mzuri, najua Yanga wanamhitaji sana lakini hakuna ubaya, tutawapa fedha wanazotaka. Kwanza Niyonzima ni mchezaji wetu, amekaa na sisi kwa miaka mingi. Tulifanya makosa kumuacha aende Yanga, kwa hiyo sasa tunamrudisha.”