Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeBusiness+PoliticsMajaji wakosoa muswada wa katiba
| + -

Majaji wakosoa muswada wa katiba

Tuesday, 15 November 2011 18:50 Deiwaka World News - Political Issues
Print PDF

Majaji wakosoa muswada wa katiba

Chama cha Majaji Wastaafu Tanzania (Tarja), kimetoa tamko kupinga hadidu za rejea za tume itakayoratibu mchakato wa kuundwa kwa Katiba Mpya kutolewa na Rais.


Tarja kimekosoa baadhi ya vifungu katika muswada huo kikiwamo kile kinachosema hadidu za rejea za Tume ya Katiba zitatolewa na Rais.

Chama hicho kimesema, hadidu za rejea zisiwe siri ya Rais kama ilivyoanishwa katika muswada huo, bali ziwekwe wazi.

Kauli hiyo ilitolewa jana Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume ya Kuchambua Muswada iliyoundwa na Tarja, Jaji Mstaafu Hamisi Msumi.

“Hadidu za rejea za tume ndiyo roho ya Katiba kwa sababu ndizo zitakazoiongoza tume kutekeleza majukumu yake,” alisema Jaji Msumi alipozungumza na waandishi wa habari.