Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeLove+RelationshipsMimba ya Wema yachoropoka
| + -

Mimba ya Wema yachoropoka

Monday, 28 November 2011 18:37 Deiwaka World News - Love+Relationships
Print PDF

Mimba ya Wema yachoropoka

Miss Tanzania 2006-07, Wema Sepetu, alikuwa na matarajio ya kuzaa na mchumba wake, Naseeb Abdul ‘Diamond’ ili kuimarisha penzi lake lakini sasa itabidi asubiri kipindi kingine.


Wema alijitangaza kuwa na mimba ya Diamond hivi karibuni lakini taarifa mpya za uhakika ni kwamba ujauzito wake umechoropoka.

Habari zinasema kuwa mimba ya Wema ilichomoka kutokana na sababu kadhaa lakini kubwa ikiwa ni ulevi wa pombe kali.

Wema amemueleza ripota wetu kuwa baada ya kugundua amenasa mimba, hakuwahi kwenda hospitali kupata ushauri wa kitaalamu, hivyo hakujua kama kunywa pombe kali ni tatizo.

Jambo lingine, Wema amesema kuwa kuna siku alipigwa na Diamond baada ya kutofautiana katika mambo yao, hivyo anahisi tatizo lilianzia hapo.

“Ni ukweli kabisa sasa hivi sina mimba, imetoka na imeniuma sana kwa sababu nilipanga kumzalia mtoto baby wangu (Diamond), nafikiri Mungu hakupanga,” alisema Wema na kuongeza: “Inauma sana lakini Mungu ndiye anayeamua.”

Wema aliendelea kusema: “Baby (Diamond) alipogundua mimba imetoka aliumia sana mpaka akalia lakini mwisho amekubali haya mambo yapo juu ya uwezo wa binadamu.”