Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeBusiness+PoliticsJK azitolea nje posho
| + -

JK azitolea nje posho

Thursday, 15 December 2011 18:00 Deiwaka World News - Political Issues
Print PDF

JK azitolea nje posho

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, amesema kuwa hawezi kuvumilia kuona taasisi za umma zikitumia mamilioni kwa ajili ya kulipa posho watumishi wake.


JK, ametoa kauli hiyo, wakati kukiwa na mjadala mzito kuhusu nyongeza ya posho za wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika maelezo yake aliyoyachapisha kwenye ukurasa wake, mtandao wa kijamii wa Facebook, JK amesema kuwa taasisi za umma, zinapaswa kutumia mali zake kwa ajili ya kujikuza na kujiboresha zenyewe.

Hata hivyo, JK, katika maelezo yake hakugusa kabisa suala la posho za wabunge ambazo ndizo gumzo kwa sasa kutokana na kuongezwa kutoka shilingi 70,000 kwa siku hadi shilingi 200,000.

Badala yake, JK, alitolea mfano Mamlaka ya Hifadhi ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) kuwa inatakiwa kujiendesha yenyewe kwa kujiboresha kupitia rasilimali zilizopo.

“Hatuwezi kuvumilia kuona taasisi za umma zikitumia mamilioni ya fedha kwa ajili tu ya posho kwa watumishi wake,” alisema JK na kuongeza:

“ Taasisi hizi kwa mfano Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) ambazo ni mali ya umma zinapaswa kutumia fedha hizi kwa ajili ya kukuza na kujiboresha zenyewe na sekta husika zaidi na zaidi na si vingineyo.”