Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeBusiness+PoliticsMaalim Seif amchimba mkwara Hamad
| + -

Maalim Seif amchimba mkwara Hamad

Sunday, 18 December 2011 05:39 Deiwaka World News - Political Issues
Print PDF

Maalim Seif amchimba mkwara Hamad

Makamu wa Kwanza wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa Chama cha Wananchi (Cuf), hakiwezi kushindwa kuchukua uamuzi mgumu inapobidi.


Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa Cuf alisema, wakati wa kuchukua uamuzi mgumu ukifika, chama chake hakitaangalia sura wala nafasi za watu kiuongozi.

Kauli hiyo ya Seif, inabeba tafsiri kwamba anamchimba mkwara Mbunge wa Wawi (Cuf), Hamad Rashid Mohamed ambaye kwa sasa ameanzisha vita ya uongozi ambayo inatishia kukigawa chama.

Hivi karibuni, Hamad ambaye alikuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani katika Bunge la Tisa, aliibua mjadala mzito ndani ya Cuf, baada ya kutangaza nia yake ya kumng’oa madarakani Seif kwa tuhuma kwamba anakiua chama.

Madai ya Hamad, yanapingwa na uongozi wa Cuf ambao unamtuhumu kutumiwa na CCM, kwa lengo la kukivuruga chama hicho.

Ndani ya Cuf, Hamad anatuhumiwa kupewa kiasi kikubwa cha fedha na kiongozi mmoja wa CCM kwa lengo la kujiimarisha kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015.

Katika maelezo yake kwa waandishi wa habari leo, Seif alisema kuwa mambo ya chama, yaachwe kwenye chama kwa sababu kuna utaratibu wake wa kuyashughulikia.

“Ndani ya Cuf hakuna mtu anazuiliwa kugombea nafasi yoyote ya uongozi. Kinachotakiwa ni kufuata utaratibu. Kugombea uongozi kuna taratibu zake,” alisema Seif.