Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeMusicVinega wakamua mbaya Arusha
| + -

Vinega wakamua mbaya Arusha

Tuesday, 20 December 2011 06:04 Deiwaka World News - Music
Print PDF

Vinega wakamua mbaya Arusha

A-Town, ilikuwa hapatoshi jana. Wapenzi wa burudani walifaidi bonge la shoo lililopomoroshwa na Vinega kibao.


Kile kilichotokea Uwanja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Dar es Salaam, kilidhihirika kwa vitendo ndani ya Uwanja wa Triple A, jana kwenye Jiji la Arusha.

Swaga za Vinega wanaosababisha kizaazaa mtaani kwa mix-tape zao za Anti Virus, zilitamba, nyomi la nguvu lilihudhuria.

Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ndiye aaliongoza shoo hiyo na Vinega wengine kibao walifanya kweli.

Shujaa wa Kundi la Wagosi wa Kaya, Fred Mariki ‘Mkoloni’, Anselm Ngaiza ‘Soggy Dog’ na mwana Hot Pot Family mwenzake, Suma G, Mapacha, Dani Msimamo, G Solo, Rama Dee, Peen Lawyer, Adili Mkwela ‘Hisabati’, D wa Geto, Magazijuto, Coin Moja na wengine kibao walifanya shoo ichangamke mbaya.