Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeSportMatumla kuchakazana tena na Osward
| + -

Matumla kuchakazana tena na Osward

Tuesday, 10 January 2012 04:43 Deiwaka World News - Sports News
Print PDF

Matumla kuchakazana tena na Osward

Mabondia wakongwe Bongo, Rashid Matumla ‘Snake Boy’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’, watapanda ulingoni tena.


Matumla na Osward, watapigana kwenye pambano lisilo la ubingwa Februari 25, mwaka huu.

Mabondia hao, wametiliana sahihi ya kukubali kutwangana Februari 25, mwaka huu ikiwa ni mechi ya marudiano katika kipindi kisichozidi miezi miwili.

Desemba mwaka jana, Matumla na Osward walipigana kwenye pambano lisilo la ubingwa lakini hakuna aliyeibuka mbabe.

Pambano hilo ambalo mabondia hao walitoka sare, lilifanyika Mtoni Kijichi, Temeke, Dar es Salaam.