Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeBusiness+PoliticsNgeleja kwenye gogoro lingine
| + -

Ngeleja kwenye gogoro lingine

Tuesday, 07 February 2012 16:07 Deiwaka World News - Political Issues
Print PDF

Ngeleja kwenye gogoro lingine

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, ameingia kwenye mgogoro mwingine kufuatia kuibuka kwa kashfa ya ufisadi ndani ya wizara yake.

Kutokana na skendo hiyo, ipo dalili kwamba watatokeza wanasiasa hususan wabunge au ujumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambao watashinikiza Ngeleja ang’oke.



Gogoro la sasa ni kwamba Wizara ya Nishati na Madini, imekumbwa na upotevu wa fedha zaidi ya shilingi bilioni 86 (dola milioni 54) ambazo ni za ununuzi wa mafuta kwenye mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura ya IPTL.

Tayari zimekwishaibuka hoja kuwa fedha hizo zimepotea kwa sababu hakuna usimamizi madhubuti kwenye wizara hiyo ambayo Ngeleja ndiye bosi mkuu akisaidiwa na naibu wake, Adam Malima.

Akiizungumzia kashfa hiyo, Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzania Bungeni, Zitto Kabwe amesema kuwa suala la ufujaji wa fedha za mafuta IPTL alilizungumza mwaka jana.

“Inasikitisha kwamba suala la ufujaji wa fedha za mafuta ya IPTL nililizungumza bungeni mwaka 2011 April. Nilimwandikia barua spika wa bunge ili jambo hilo lifanyiwe uchunguzi maalum na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.

“Kuchelewa kushughulikia jambo hilo kunazidisha hasara kwa taifa na fedha kidogo za umma zinazopatikana zinakwenda kwenye mifuko ya wajanja wachache. Hivi haiwezekani nchi hii ikawa haina drama za ufisadi?

“Hasa Wizara hii ya Nishati na Madini? Spika aruhusu uchunguzi huu haraka na wahusika washtakiwe na mali zao walizopata kwa njia hii haramu zinyanganywe.”