Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeSportKagera Sugar ni katafunua na Oljoro
| + -

Kagera Sugar ni katafunua na Oljoro

Monday, 05 March 2012 05:02 Deiwaka World News - Sports News
Print PDF

Kagera Sugar ni katafunua na Oljoro

Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ambayo iko katika mzunguko wa pili imeendelea tena leo (Machi 2 mwaka huu) na kesho (Machi 3 mwaka huu) baada ya kusimama kwa wiki moja kupisha mechi kati ya timu ya Taifa (Taifa Stars) dhidi ya Msumbiji (Mambas).

Leo kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam kulikuwa na mechi kati ya JKT Ruvu na Toto Africans.

Mechi za kesho (Machi 3 mwaka huu) ni kati ya Oljoro itakayokuwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.

Nayo Polisi Dodoma ikiwa chini ya makocha Rashid Chama na Henry Mkanwa itakuwa ugenini kwenye mashamba ya miwa ya Mtibwa mjini Turiani kuikabili Mtibwa Sugar ya huko.

Machi 5 mwaka huu Moro United inayofundishwa na Hassan Banyai itaoneshana kazi na JKT Ruvu ambayo iko chini ya Charles Kilinda katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.

Mechi za Machi 7 mwaka huu ni kati ya Oljoro na Toto African (Sheikh Kaluta Amri Abeid), Simba na Kagera Sugar (Uwanja wa Taifa) wakati Azam itakuwa mwenyeji wa Coastal Union kwenye Uwanja wa Chamazi.