Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeBusiness+PoliticsSinema kamili ya Waziri Malima kuibiwa hotelini
| + -

Sinema kamili ya Waziri Malima kuibiwa hotelini

Tuesday, 13 March 2012 05:14 Deiwaka World News - Political Issues
Print PDF

Sinema kamili ya Waziri Malima kuibiwa hotelini

Sakata la Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Kighoma Malima kulizwa fedha na mali zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 23 hotelini, mwishoni mwa wiki iliyopita liligeuka sinema mjini Morogoro’.

TAARIFA YA POLISI

Kwa mujibu wa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa wa Morogoro, Hamis Seleman, katika tukio hilo, chumba alichopanga Malima kwenye hoteli hiyo ya kifahari ya Nashera iliyopo mjini hapa, kilivunjwa na kuibwa mabegi matatu yenye kompyuta mbili ndogo, simu tatu za mkononi na vitu mbalimbali.

Pia, taarifa ya polisi ilieleza kuwa mbali na mabegi hayo, Malima aliibiwa fedha taslimu Shilingi milioni 1.5 na dola za Kimarekeni taslimu 4,000 pamoja na pasipoti yake.

Kamanda Seleman alisema dirisha la chumba hicho lilivunjwa na wezi kuingia na kuiba mabegi hayo zikiwemo kompyuta hizo aina ya Dell zenye thamani ya jumla ya Sh milioni 5.5.

Kwa mujibu wa Seleman, Naibu Waziri aligundua kuvunjwa kwa dirisha na kuibiwa vitu hivyo, baada ya kuingia ndani akitokea sebuleni alikokuwa amejipumzisha awali.

Alivitaja vitu vingine vilivyokuwa ndani ya mabegi hayo kuwa ni vinasa sauti vitatu vyenye thamani ya Sh. milioni moja, simu tatu aina tofauti zenye thamani ya jumla ya Sh. milioni 1.3, pete mbili za fedha zenye thamani ya jumla ya Sh. milioni 2.5, kadi za benki ‘ATM’ na kofia aina ya baraghashia yenye thamani ya Sh 50,000.

Kwa mujibu wa Seleman, wezi hao waliacha bastola moja na bunduki na upelelezi unaendelea huku walinzi watatu wa hoteli hiyo wakishikiliwa na polisi.

Baada ya taarifa hiyo ya kipolisi na ishu hiyo kuwa gumzo, ripota wetu alizama mzigoni ambapo alikwenda kupiga kambi hotelini hapo.

Ili kujua kama kuna habari nyuma ya pazia, ripota wetu alimuomba Malima kupekua chumba kona hadi kona huku likipata ufafanuzi kwa kila kilichokuwemo.

ASIMULIA HUKU AKICHAMBUA VITU CHUMBANI

“Niliangalia taarifa ya habari nikaona ni vema nikaandika baadhi ya maazimio niliyoyatoa kwenye mkutano wangu na wadau wa sekta ya madini.

“Nikiwa hapa (akionesha sehemu aliyokuwa amekaa), nilipitiwa na usingizi hadi niliposhituka saa 10.45 alfajiri na kawaida muda huo usingizi huniruka kwa sababu ya kuamka kwenda kuswali, nilishituka nikajiuliza simu zangu ziliko na kubaini kuwa niliziacha chumbani.

“Nilipoingia chumbani sikuziona na hata sebuleni hazikuwapo, nilipotazama huku na kule mabegi nayo sikuyaona, moja la laptop na lingine la majalada.

“Niligundua kuna mtu aliingia kwa sababu niliona matope na nilipoyafuatilia nikagundua ni nyayo za mtu.

“Nilijua kuna mtu ameniibia lakini cha ajabu silaha ameniachia kwa hiyo nimeibiwa mabegi yangu matatu, moja lina kompyuta, mawili yana nyaraka.

“Nilitoka kwenda kuwataarifu watu wa mapokezi nao wakampa taarifa meneja.

“Ukweli nimeibiwa vitu vya thamani sana, laptop mbili, simu, pia pete mbili hizi zina thamani, moja nimeachiwa na marehemu baba yangu, hiyo kwangu ina thamani sana, haina thamani ya fedha ila na mimi nikiondoka duniani ni urithi wa familia, nyingine ni ya mke wangu.

Pamoja na simulizi yake hiyo mithili ya muvi, ripota wetu alimuweka ‘mtukati’ ndani ya chumba hicho ambapo mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo;

SWALI: Mazingira ya tukio lililokupata yana utata sana huko mtaani, je, unadhani ulikuwa na ulinzi imara au hafifu.

MALIMA: Najua baada ya tukio hili yatasemwa mengi, kwamba nimeibiwa kila kitu hadi nguo za ndani, ukweli ni kwamba nguo zangu zote zipo (huku akichambua moja baada ya nyingine kwenye begi), ikiwemo tisheti yangu ya Timu ya Taifa yenye jina langu (anaitoa).

“Nakumbuka nilifika hapa hotelini saa 5:00 usiku, nilikuwa na kikao kwa mkuu wa mkoa (Joel Bendera) baada ya kutoka kwenye ziara yangu kule Matombo.

SWALI: Lakini mheshimiwa sehemu yenyewe aliyopitia mwizi ni finyu, ina maana hukusikia chochote wakati anachambua vitu na kukuachia baadhi?

MALIMA: Siyo kweli hizo ni hisia zako. Nilikuwa na uchovu wa safari ndefu, ndiyo uliochangia mimi kutomsikia.