Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeBusiness+PoliticsJK awaapisha makatibu tawala Ikulu
| + -

JK awaapisha makatibu tawala Ikulu

Sunday, 25 March 2012 05:17 Deiwaka World News - Political Issues
Print PDF

JK awaapisha makatibu tawala Ikulu

Rais Jakaya Kikwete, leo amewaapisha makatibu tawala wapya wa mikoa mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, JK amewaapisha makatibu tawala wapya wa mikoa saba nchini.

Taarifa kwa vyombo vya habari imechambua kwamba aliyeapishwa kuwa Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Mbeya ni Mariam Mtunguja.

Wengine walioapishwa na majina yao kwenye mabano ni Faisal Issa (Kilimanjaro), Bwana Eliya Ntandu (Morogoro), Bwana Severine Kahitwa (Geita), Bwana Emmanuel Kalobelo (Katavi), Bwana Hassan Bendeyeko (Ruvuma) na Dkt. Anselem Tarimo (Shinyanga).