Amanda adai kutokuzaa ni siri yake
Msanii wa filamu Bongo, Amanda Posh amefunguka kuwa licha ya mengi kuzungumzwa kufuatia kuwepo kwenye ndoa kwa muda mrefu bila mtoto, yeye ana siri ya kutozaa kwa sasa.
Amanda amesema, amekuwa akisikia maneno chinichini kuwa yeye hazai bila watu kujua kuwa uwezo huo anao ila ni ishu ya kujipanga tu.

“Siri ya kwa nini sizai kwa sasa ninayo mwenyewe ila siyo kweli kwamba sina uwezo wa kubeba mimba. Na kwa wasiojua nilishawahi kubeba mimba, mtoto akafia tumboni,” alisema Amanda na kuongeza:
“Ni kweli nina miaka mitatu ndani ya ndoa lakini mimi na mume wangu tumeamua tutulie kabla ya kuamua kuleta kiumbe duniani na siku nikiwa na mimba hakuna atakayejua, watashangaa nimejifungua tu.”