Man City yaibonda Man U
Bao la dakika la 45, lililowekwa kimiani ni nahodha wa Manchester City, Vincent Kompany limeizamisha jumla Manchester United.

Licha ya kujitahidi kukukuruka, hadi mwisho wa mchezo Man United ililala kwa bao hilo moja.
Kwa matokeo hayo, Man City imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England.
City inakamata kilele kutokana na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Timu hizo, sasa zinalingana pointi na zimebakisha mechi mbili kila moja kabla ya kutangaza ubingwa.