Mume, mke wa mtu wagandana wakizini
Unaamini katika ndumba? Tukio la kustaajabisha limetokea nchini Kenya ambapo mke wa mtu, aliyekuwa anazini na mume wa mtu, walikutwa wamegandana.
Wawili hao baada ya kumaliza haja zao, kila walipojaribu kuachiana ilishindikana mpaka watu waliposhtukia tukio hilo na kuvamia chumbani.

Polisi walisimamia tukio hilo ambalo lilikusanya umati mkubwa wa watu.
Inadaiwa kuwa mume wa mwanamke huyo, aliweka mtego wa dawa za asili kwa mkewe ambao ulifanikisha fumanizi hilo.
Mtego huo ni kwamba amemtega mkewe kimazingara, hivyo popote atakapokwenda kuzini ni lazima akamatwe kwa mtindo wa kugandana na atakayezini naye.
Jitihada zilifanyika kuwaachanisha wagoni hao lakini ilishindikana licha ya kumtumia mchungaji aliyeshusha neno zito.
Mume wa mwanamke huyo alikuwepo, baadaye alitoa sharti la kupewa shilingi 20,000 za Kenya na baada ya kukabidhiwa, wagoni hao waliachiana.
Ufafanuzi zaidi wa tukio hilo, tazama video hii.