Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeLifestyle+FashionHali ya Sajuki yazidi kuliza wengi
| + -

Hali ya Sajuki yazidi kuliza wengi

Saturday, 12 May 2012 17:50 Deiwaka World News - Lifestyle+Fashion
Print PDF

Hali ya Sajuki yazidi kuliza wengi

Siku mbili kabla ya kwenda katika Hospitali ya Apollo nchini India kwa matibabu, afya ya stadi wa filamu za Kibongo, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ni ya kusikitisha kupitiliza.

Kadiri siku zinavyosonga, hali ya Sajuki inazidi kuwatoa watu machozi baada ya kuzidiwa na kushindwa kunyanyuka kitandani.

ASHINDWA KUPOKEA MCHANGO

Tukio bichi kabisa lililowatoa machozi wasanii wenzake ni lile la Jumanne wiki hii nyumbani kwake Tabata Barakuda, Dar es Salaam ambapo msanii na prodyuza huyo wa filamu alishindwa kuamka kitandani kupokea dola elfu kumi (takribani Sh. milioni 15) alizozitoa mwigizaji mwenzake, Jacqueline Wolper kwa ajili ya matibabu huku akisindikizwa na mastaa wengine wa Bongo Movie.

Ripota wetu alimshuhudia Sajuki akiugulia maumivu huku akilalamika kujisikia vibaya, hivyo kuwaomba wasanii wenzake kwa heshima waingie chumbani kwake ili apokee fedha hizo.

WASANII VILIO

Kitendo hicho ndicho kilichowafanya baadhi ya wasanii wenzake kushindwa kujizuia na kujikuta wakiangua vilio huku Sajuki akiwatuliza na kuwaomba wasilie wala wasihuzunike kwani kila kitu ni mapenzi ya Mungu.

“Msihuzunike ndugu zangu, naamini kila kitu ni mapenzi ya Mungu na si vinginevyo, jipeni moyo,” alisema Sajuki kwa tabu akiwa amelala kitandani akiwa amezungukwa na mastaa hao.

WOLPER

Kwa upande wake Wolper aliyekuwa akimwaga machozi mithili ya bomba la mvua, alisema kuwa siyo kwamba ana fedha nyingi, ila ni namna alivyoguswa na mateso ya Sajuki.

“Siyo kwamba sina shida bali ni moyo wa kusaidia kuokoa uhai wa mwenzetu. Tulizoea kuwa naye location (sehemu ya kurekodia filamu) na kwenye tasnia yetu, anaumwa na hajiwezi, niliumia sana,” alisema Wolper aliyekuwa akifutwa machozi na wenzake.

WASTARA

Naye mke wa Sajuki, Wastara Juma, huku akilia muda wote, alitoa shukurani zake za dhati kwa Wolper na kueleza jinsi alivyoguswa na kuona umuhimu wa kumsaidia mumewe.

MASTAA

Baadhi ya mastaa wa Bongo Movie walioambatana na Wolper kuwasilisha mchango huo ni pamoja na Jacob Steven ‘JB’, Muhsein Awadhi ‘Dk. Cheni’, Chiki Mchoma ‘Chiki’, Hartmann Mbilinyi, Sabrina Rupia ‘Cathy’ na wengine.

HISTORIA UGONJWA WA SAJUKI

Taarifa za awali kabla ya Sajuki kuthibitisha ilielezwa kuwa alianza kwa kupata uvimbe sehemu tofauti katika mkono wake mmoja lakini baadaye tatizo hilo lilihamia ndani na kuanza kupata maumivu makali pembeni ya ini.