Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeLifestyle+FashionArobaini ya Kanumba utata
| + -

Arobaini ya Kanumba utata

Friday, 18 May 2012 18:56 Deiwaka World News - Lifestyle+Fashion
Print PDF

Arobaini ya Kanumba utata

Tangu staa wa filamu Bongo, Steven Charles Kanumba ‘The Great’, afariki dunia, leo ni siku ya 40 lakini giza nene linaonekana kuigubika shughuli hiyo kufuatia tamko la mama wa marehemu.

Mama wa marehemu, Flora Mtegoa alisema ni kweli arobaini imefika lakini hajui kinachoendelea ila itafanyika Mei 20, 2012.

TAMKO LA MAMA

Mama Kanumba alikuwa akijibu swali la kipaparazi lililomtaka afafanue kama mkusanyiko wa arobaini ya marehemu utakuwepo au kila mtu atakuwa kivyake.

“Nimeambiwa itafanyika tarehe 20 mwezi huu lakini zaidi ya hapo sijui chochote kile kinachoendelea mwanangu,” alisema mama huyo kwa sauti iliyojaa unyenyekevu.

HABARI NDANI YA TASNIA YA SINEMA

Mmoja wa wasanii wa filamu za Kibongo ambaye hakupenda jina lake liwekwe wazi. Yeye alikuwa na haya ya kusema:

“Ilibidi arobaini yake ifanyike Mei 17 (leo) lakini kila tukiulizia tunaambiwa mipango bado haijakamilika, mipango gani hiyo kama fedha zilipatikana nyingi sana katika rambirambi.

“Wanaona hasara kuzitoa kwa ajili ya kununulia vifaa vya arobaini?”

Aidha, msanii huyo aliitaka kamati ya maandalizi ya arobaini hiyo (kama ipo) kutoifanya kienyeji na kushauri kuwa inabidi itangazwe ili watu wahudhurie kwa wingi kama siku ya mazishi.

“Kinachoonekana wanataka kufanya shughuli bora ifanyike, watakuwa wameharibu sana. Wakifanya shughuli kubwa pengine hata rais au mawaziri na wabunge wanaweza kuhudhuria,” alisema msanii huyo.

MANENO YA JB

Msanii Jacob Steven JB, Mwenyekiti wa Bongo Movie, alisema hajui lolote kuhusu arobaini hiyo.

Akasema: “Kwa taarifa nzuri labda muulize Gabriel Mtitu ‘Mtitu Game’ (aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maziko), yeye atakuwa anajua lolote.”

SAUTI YA MTITU GAME

Mtitu Game alisema: “Aaa, yeah! Arobaini imeangukia Alhamisi, siku ya kazi. Kwa hiyo familia ikaona ifanyike Mei 20, mwaka huu ambayo itakuwa Jumapili,” alisema Mtitu na kuongeza:

“Kutakuwa na ibada pale Kanisa la AIC Chang’ombe, halafu baadaye wanandugu watakusanyika nyumbani kwa marehemu (Sinza) kwa ajili ya chakula cha pamoja.”

BABA KANUMBA NAYE

Baba mzazi wa marehemu, Mzee Charles Kanumba alisema: “Sijajua, ila lazima iwepo. Mama Kanumba anajua kila kitu, akisema hajui lolote ni janja ya nyani tu. Mimi najiandaa kuja huko siku mbili hizi, nikifika kila kitu kitajulikana.”