Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeLifestyle+FashionNamna bora ya kuvaa unapoalikwa harusini
| + -

Namna bora ya kuvaa unapoalikwa harusini

Sunday, 20 May 2012 20:45 Deiwaka World News - Lifestyle+Fashion
Print PDF

Namna bora ya kuvaa unapoalikwa harusini

Ni jambo la kawaida mtu kuvaa t-shirt na jeans anapokwenda harusini. Kila mtu yupo huru kuvaa anavyopenda lakini hapa kuna ushauri kiduchu kuhusu uvaaji harusini.

Wapo wanawake ambao nao huvaa jeans waendapo kwenye mitoko ya harusi. Hao huchemka zaidi.

Harusi ina mandhari yake, kwa hiyo kuna mavazi ambayo ukiyatinga, utakuwa umekwenda sawa na eneo la tukio.

SI KILA JEANS HAIFAI

Jeans hatakubalika endapo itaunganishwa na t-shirt. Endapo utavaa jeans na shati, ukizingatia rangi, utapendeza.

Mfano, jeans nyeusi, blu au kijivu na shati jeupe, kijivu, maruni na kadhalika, chomekea halafu unganisha na tai. Hapo utapendeza kama utazingatia rangi.

Mwanamke anaweza kuvaa jeans lakini kinachoangaliwa ni lile vazi la juu. Kama t-shirt au shati, haipendezi. Unaweza kupendeza lakini ukawa huendani na mandhari.

Vaa jeans halafu tinga gauni linaloishia kwenye magoti. Zingatia rangi na utapendeza.

Picha zifuatazo ni mfano wa mtu anayeweza kuvaa anapoalikwa harusini.