Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeSportMambo yanoga sherehe za ubingwa Simba
| + -

Mambo yanoga sherehe za ubingwa Simba

Saturday, 26 May 2012 06:59 Deiwaka World News - Sports News
Print PDF

Mambo yanoga sherehe za ubingwa Simba

Klabu ya mpira wa miguu ya Simba leo imezungumzia juu ya sherehe ya ubingwa wa kombe la Tanzania Bara 2012 walilolitwaa hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari, Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, alisema maandalizi ya sherehe hiyo tayari yameshakamilika na kinachosubiriwa hadi sasa ni siku husika ambayo ni Jumapili ya wiki hii, tarehe 27.

Alisema wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo watatakiwa siku ya Jumapili hii kukusanyika makao makuu ya klabu hiyo, Mtaa wa Msimbazi, asubuhi tayari kwa safari ya kuelekea katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam, ambapo sherehe hizo zitafanyika.