Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeLifestyle+FashionMiss Chang’ombe kuwaka moto kesho
| + -

Miss Chang’ombe kuwaka moto kesho

Friday, 08 June 2012 10:00 Deiwaka World News - Lifestyle+Fashion
Print PDF

Miss Chang’ombe kuwaka moto kesho

Warembo 14 (baadhi yao pichani) kesho watatoana jasho katika kinyang’anyiro cha kumsaka Malkia wa Chang’ombe 2012, shindano litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Quality Centre uliopo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa shindano hilo, Tomas Chilala ‘Tom’ alisema kuwa kila mrembo ametamba kuwafunika wenzake siku hiyo.

Chilala aliongeza kuwa shindano hilo litakwenda sambamba na burudani kutoka kwa msanii Diamond na Mapacha Watatu ambao wameahidi kutoa shoo ya kiwango cha juu.

“Kwa upande wangu maandalizi yote yameshakamilika, tunaisubiri tu hiyo kesho ifike ili tumpate Malkia wa Chang’ombe wa mwaka huu,” alisema Chilala.