Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeSportShomari Kapombe aongezewa ulaji Simba
| + -

Shomari Kapombe aongezewa ulaji Simba

Thursday, 14 June 2012 16:23 Deiwaka World News - Sports News
Print PDF

Shomari Kapombe aongezewa ulaji Simba

Baada ya beki, Kelvin Yondani kuondoka Simba, kinda wa timu hiyo, Shomari Kapombe, ameanza kupewa mshahara aliokuwa akilipwa mkongwe huyo.

Yondani hivi karibuni alisaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga kwa dau la shilingi milioni 30.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya benchi la ufundi la Simba, mshahara aliokuwa akilipwa Yondani ambao ni Sh 800,000 umehamishiwa kwa Kapombe.

Awali, Kapombe alikuwa na mshahara usiofikia Sh 500,000 lakini sasa anapata mshahara kama ule aliokuwa akilipwa Yondani, yaani Sh 800,000.

“Kama kamati tumetoa mapendekezo ya kumboreshea mshahara Kapombe kwa ajili ya kumpa morali zaidi, hivi sasa atakuwa akilipwa shilingi 800,000.

“Kiasi hicho alikuwa akilipwa Yondani, tumeona tumhamishie kiasi hicho baada ya kuridhishwa na kiwango chake,” kilisema chanzo hicho.

Kapombe alionyesha kiwango cha kuvutia msimu uliopita, ukiwa ni msimu wake wa kwanza kukichezea kikosi cha kwanza cha Simba lakini sifa yake kubwa ni uwezo wa kucheza namba karibu zote uwanjani ‘kiraka’.

Hata hivyo, wikiendi iliyopita aliwika tena akiwa na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.