Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeBusiness+PoliticsKangi ajiandaa kumlipua January Makamba
| + -

Kangi ajiandaa kumlipua January Makamba

Monday, 18 June 2012 09:21 Deiwaka World News - Political Issues
Print PDF

Kangi ajiandaa kumlipua January Makamba

Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugora, anadaiwa kujiweka chimbo akiandaa makombora dhidi ya Mbunge wa Bumbuli, aliye pia Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.

Vyanzo vyetu vimeweka kweupe kuwa Kangi anataka kumlipua January ili kulipa kisasi, baada ya mbunge huyo wa Bumbuli kumkaanga kwenye kikao cha wabunge wa CCM, kilichofanyika jana bungeni kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa.

Katika kikao hicho, January alitaka Kangi aadhibiwe kwa kile alichokiita kwamba anakisaliti chama na pale mbunge huyo wa Mwibara alipotaka kusimama kujibu mapigo, alinyimwa nafasi hiyo.

Kikao hicho, kiliketi chini ya mwenyekiti wa wabunge wa CCM, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na madhumuni yake yalikuwa kuwashawishi wabunge wote wa CCM kuipitisha bajeti iliyosomwa Alhamisi iliyopita na Waziri wa Fedha, William Mgimwa.

“Mheshimiwa Kangi siyo mtu wa kutulia hivihivi, sasa hivi anajiandaa kurusha makombora kwa January. Ile hali ya kunyimwa kujibu mapigo ukumbini, aliichukulia kama amenyimwa haki yake ya kimsingi, kwa hiyo anajiandaa kujibu mapigo,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:

“Tupo karibu na Kangi, tunajua lazima amfyatue Makamba. Unajua Kangi ni mtu mwenye msimamo madhubuti ndiyo maana baada ya kunyimwa fursa ya kuzungumza pale ukumbini, aliondoka zake.”