Diamond, Chameleon kusaka mkali wa steji
Wakali wa kushambulia jukwaa ukanda wa Afrika Mashariki, Joseph Mayanja na Nasibu Abdu Juma ‘Diamond’, wataoneshana nani mkali wa steji kwenye Tamasha la Usiku wa Tumaini ambalo litafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Mratibu wa tamasha hilo, Abdallah Mrisho amesema kuwa Diamond amekuwa akisifika kwa kufanya shoo kali nchini hivi sasa, wakati Chameleon anakubalika uwezo wake kwa muda mrefu, hivyo shoo hiyo itamaliza ubishi.
“Tunataka kuonesha kwa vitendo ni nani mkali wa kumiliki jukwaa kati ya Chameleon na Diamond,” alisema Mrisho na kuongeza: “Siku hiyo kweli utakuwa Usiku wa Tumaini kwa maana tunatarajia kufanya mengi makubwa.”
Mrisho aliongeza kuwa siku hiyohiyo, staa wa Hip Hop nchini, Ibrahim Mussa Mshana ‘Roma’, atashuka jukwaani kuwadatisha watu watakaohudhuria.
Click here for TUMA Registrations.