Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeMusicDiamond anunua mkoko wa bei mbaya
| + -

Diamond anunua mkoko wa bei mbaya

Wednesday, 20 June 2012 05:18 Deiwaka World News - Music
Print PDF

Diamond anunua mkoko wa bei mbaya

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdu Juma ‘Diamond’, amenunua mkoko wa bei mbaya.

Mkoko huo aina Toyota Land Cruiser Prado, Diamond ameanza kuutumia rasmi leo na bado hajakamilisha hata taratibu za kuusajili.

Hii inathibitisha mafanikio yake kimuziki, kwani imekuwa ikielezwa tu kwamba ni msanii wa muziki Bongo anayeingiza mkwanja mkubwa hivi sasa.

Diamond mwenyewe akizungumza na ripota wa site hii, amesema kuwa mkoko huo umemgharimu shilingi milioni 75 kuunua, kuusafirisha, kulipia ushuru hadi kuumiliki.

“Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kununua gari hili, linamaanisha kitu kikubwa sana katika maisha yangu,” alisema Diamond.