Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeBusiness+PoliticsMnyika atimuliwa bungeni
| + -

Mnyika atimuliwa bungeni

Wednesday, 20 June 2012 05:37 Deiwaka World News - Political Issues
Print PDF

Mnyika atimuliwa bungeni

Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, ametimuliwa bungeni leo.

Mnyika, alifukuzwa bungeni na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, baada ya kuzungumza kile kilichotafsiriwa kwamba ni maneno ya kuudhi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.

Mbunge huyo kijana ambaye ni Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, alitakiwa kufuta kauli hiyo na Ndugai lakini akagoma, hivyo akaamriwa kutokanyaga viwanja vya bunge mpaka kesho asubuhi.

Katika kauli yake, Mnyika alisema kwamba Rais Kikwete ni dhaifu na alipotakiwa kufuta kauli yake alijibu: “Kauli yangu kwamba rais ni dhaifu sitaifuta.”